Utomvu ni kiowevu kinachopitishwa katika seli za mimea. Unasafirisha maji na lishe ndani ya mmea[1].
Kutokana na aina mbili tofauti za seli za mimea, yaani zilemu na floemu, kuna aina mbili za utomvu wa zilemu na utomvu wa floemu[2].
Utomvu wa zilemu ni mmumunyo wa maji na homoni, madini na lishe nyingine, Mwendo wake ni kutoka mizizi kuelekea kwenye majani.
Utomvu wa floemu ni mmumunyo wa maji na sukari, homoni na madini. Inashuka kutoka sehemu ambako kabohaidreti na sukari zinalishwa kwenda pale zinapohitajika, yaani kwenye sehemu ambako mmea unakua au sehemu ambako kabohaidreti zinatunzwa kama akiba.
Watu wametumia aina za utomvu, hasa ya floemu, tangu kale.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Utomvu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |