Mt. Alfege.

Alfege wa Canterbury (jina lake huandikwa pia “Aelfheah”; takriban 95419 Aprili 1012) alikuwa mkaapweke, halafu abati wa monasteri, askofu na hatimaye askofu mkuu wa Canterbury nchini Uingereza.

Mwaka 1011, wakati wa uvamizi wa kikatili wa maharamia Wadenmark, alijitoa badala ya waumini wake akakamatwa, na kwa kuwa alikataa kukombolewa kwa pesa, Jumamosi baada ya Pasaka alipigwa kwa mifupa ya kondoo na hatimaye alikatwa kichwa kwenye kingo ya mto Thames, karibu na Greenwich[1].

Alitambuliwa rasmi kuwa mtakatifu mfiadini na Papa Gregori VII mwaka 1078.

Sikukuu yake ni tarehe 19 Aprili[2].

Tazama pia

Tanbihi

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/91288
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo

      .
     . http://www.oxforddnb.com/view/article/181. Retrieved 7 Novemba 2007.

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Alfege wa Canterbury
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.