Mchoro mdogo wa Mt. Anfiloki.

Anfiloki wa Ikonio (alizaliwa Kapadokia, leo nchini Uturuki, 340 hivi - Konya, Likaonia 403 hivi) alikuwa mmonaki, askofu wa Konya kuanzia mwaka 374 na mwanateolojia maarufu, ndugu wa Gregori wa Nazianzo na rafiki wa Basili Mkuu [1].

Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu na mmojawapo kati ya mababu wa Kanisa.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 23 Novemba[2].

Maandishi

Maandishi yake mengi yamepotea. Zimebaki hotuba 8, barua kwa Sinodi ya Ikonio[3] na labda zaidi kidogo.

Tazama pia

Tanbihi

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/93189
  2. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
  3. Goldhorn, S. Basil., Opp. Sel. Dogm., 630-635.

Vyanzo

Marejeo

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.