Mchoro wa Mtaguso wa kwanza wa Nisea ukimuonyesha Ario chini ya mihuu ya Kaisari Konstantino Mkuu na maaskofu.

Ario (kwa Kiberberi: Aryus ; kwa Kigiriki Ἄρειος, Areios, 250 au 256336) alikuwa padri kutoka Libya aliyefanya kazi huko Alexandria, Misri.[1]

Mafundisho yake[2][3] yalisisitiza kuwa Mungu Baba ni mkuu kuliko Mwana,[4] akipinga imani katika Utatu.[5]

Kristolojia yake ilikanushwa na askofu wake, Aleksanda wa Aleksandria, lakini ilienea kote mashariki mwa Dola la Roma na kuvuruga Kanisa Katoliki kiasi cha kudai Kaisari Konstantino I aitishe Mtaguso wa kwanza wa Nisea mwaka 325.

Huo mtaguso mkuu wa kwanza, uliokusanya maaskofu wengi hasa wa mashariki, ulikataa hoja zake na kumkiri Mwana kuwa na hali ileile ya Baba.

Hata hivyo vurugu ziliendelea hata kudai ufanyike mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (383), ambao ni wa pili kati ya mitaguso ya kiekumene, nao ukasisitiza na kukamilisha imani ya mtaguso wa kwanza wa Nisea katika Kanuni ya Imani ya Nisea-Konstantinopoli.

Ingawa imani hiyo ilikubaliwa kura rasmi katika Dola la Roma, Uario ulienea kati ya makabila ya Kijerumani, hasa Wagoti na Wavandali, hivyo uliendelea hadi karne ya 7 na ya 8.

Mpaka leo kuna madhehebu yanayokanusha umungu wa Yesu Kristo na kusema ni kiumbe tu.

Maandishi yake

Tanbihi

  1. Anatolios, Khaled (2011). "2. Development of Trinitarian Doctrine: A Model and Its Application". Retrieving Nicaea. Grand Rapids: BakerAcademic. uk. 44. ISBN 080103132X. Arius, who was born in Libya, was a respected ascetic and presbyter at the church of the Baucalis in Alexandria. 
  2. Hanson, R P C (2007). The Search for the Christian Doctrine of God. Grand Rapids: Baker Academic. ku. 127–128. ISBN 0-8010-3146-X. 
  3. Kopeck, M R (1985). "Neo Arian Religion: Evidence of the Apostolic Constitutions". Arianism: Historical and Theological Reassessments: 160–162. 
  4. Williams, Rowan (2002) [1987]. Arius (toleo la Revised). Grand Rapids, Mich: W.B. Eerdmans. uk. 98. ISBN 0-8028-4969-5. 
  5. Constantine the Great Rules Archived 21 Novemba 2017 at the Wayback Machine. - National Geographic - Retrieved 23 September 2014.

Marejeo

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ario kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.