Bunge la Tanzania ni baraza la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linalotunga sheria na kuisimamia serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.
Bunge linamjumuisha rais wa Tanzania pamoja na wabunge. Mnamo mwaka 2017 kulikuwa na wabunge 393[1] wanaoingia kwa namna tofauti [2]
Mamlaka ya Bunge iko juu ya mambo yote yasiyo ya Zanzibar pekee.
Kuna majimbo 214 Tanzania Bara na majimbo 50 Zanzibar.
Majimbo yanatofautiana kwa kiasi kikubwa katika idadi ya wakazi. Wastani wa Tanzania bara ni mbunge mmoja kwa wakazi 227,461. [3] Kuna majimbo katika mikoa ambako mbunge mmoja anawakilisha watu wengi zaidi kama vile Dar es Salaam (wakazi 546,542/mbunge 1), Mwanza (346,999) na Kagera (309,953). Kinyume chake kuna majimbo mengine ambako mbunge anawakilisha watu wachache kama vile Pwani (wakazi 133.104/mbunge), Katavi (128.513), Njombe (120.795) au Lindi (112.192).
Tofauti ni kubwa zaidi huko Zanzibar. Kwa mfano Wilaya ya Kaskazini B katika Mkoa wa Unguja Kaskazini ina wakazi 81,675[4] pekee lakini inachagua wabunge 4 katika majimbo ya Bumbwini, Donge, Kiwengwa na Mahonda.
Bunge linatekeleza kazi yake kwa kiasi kikubwa kupitia kamati mbalimbali. Kuna aina tofauti za kama kama vile:
Kamati za kudumu zinazohusu uendeshaji wa Bunge:
Kamati za kudumu za Bunge za Kisekta
Kamati za Sekta Mtambuka:
Kamati za kudumu za Bunge zinazosimamia matumizi ya fedha za Umma: