Chande
Spishi ya chande akionyesha miguu mirefu minane yake.
Spishi ya chande akionyesha miguu mirefu minane yake.
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Faila: Arthropoda
Nusufaila: Chelicerata
Ngeli: Arachnida
Oda: Opiliones
Ngazi za chini

Nusuoda 5:

  • Cyphophthalmi
  • Dyspnoi
  • Eupnoi
  • Laniatores
  • †Tetrophthalmi

Chande ni arithropodi wa oda Opiliones katika ngeli Arachnida wafananao na buibui. Kama hao chande wana miguu minane, lakini miguu yao ni mirefu sana katika spishi nyingi. Jozi ya pili ni mirefu kuliko mingine na hutumika kama vipapasio. Sehemu zote za mwili wao zimeungana, kwa hivyo hakuna finyo kati ya kefalotoraksi na fumbatio kama kwa buibui, lakini kama hao wana kelisera (chelicera) na pedipalpi. Hawawezi kukalidi nyuzi za hariri, kwa hivyo hawatengenezi utando. Wana macho mawili tu (buibui wana 6 au 8).

Spishi nyingi hula vitu vingi (omnivores): wadudu wadogo, dutu ya mimea, kuvu, mizoga midogo na mavi. Chande wawindaji wengi huvizia mawingo, lakini wengine huwinda wakikimbia.

Spishi za Afrika ya Mashariki

Picha