Chunusi | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Specialty | Dermatology, family medicine ![]() |
ICD-10 | L70.0 |
ICD-9 | 706.1 |
DiseasesDB | 10765 |
MedlinePlus | 000873 |
eMedicine | derm/2 |
MeSH | D000152 |
Chunusi (kutoka kitenzi "chunuka"; kwa Kilatini na Kiingereza: acne vulgaris) ni hali ya muda mrefu ya ngozi inayodhihirika kwa madoa meusi, madoa meupe, ngozi yenye mafuta na wakati mwingine kovu.[1][2]
Sura ya mtu baada ya kupata chunusi inaweza kumsababishia wasiwasi, kiwango cha chini cha kujithamini na katika visa vikali zaidi fadhaiko au hata mawazo ya kujiua.[3][4]
Jina la Kiswahili linadokeza imani ya kale ya kwamba chunusi ilitokana na kijana kutunukwa (kutokea kupendwa) na mwingine. Kumbe maelezo ya sayansi ni kama ifuatavyo.
Jeni zinakadiriwa kusababisha asilimia 80 za visa hivyo.[2] Si dhahiri kama lishe husababisha hali hii.[2] Hakuna ushahidi wa manufaa ya usafi wala miale ya jua.[2]
Hata hivyo uvutaji sigara huongeza hatari ya kupata chunusi na kuzidisha ukali wake.[5]
Chunusi mara nyingi huathiri ngozi na idadi kubwa ya tezi za mafuta ikijumuisha uso, sehemu ya juu ya kifua na mgongo.[6]
Wakati wa kubalehe kwa jinsia zote mbili, chunusi mara nyingi husababishwa na ongezeko la androjeni kama vile testosteroni.[7]
Kuna njia nyingi za matibabu za kupunguza chunusi zikijumuisha kubadili hali ya maisha, taratibu na dawa. Kula kabohidrati chache na zinazomeng’enywa kwa urahisi, kama vile sukari, kunaweza kusaidia.[8]
Benzoyl peroxide, asidi ya salicili, na asidi ya azela ya kupaka ni dawa zinazotumika mara nyingi.[9] Antibiotiki na retinoidi za kupaka na za kumeza hutumika kutibu chunusi.[9] Hata hivyo, ukinzani dhidi ya antibiotiki unaweza kutokea.[10]
Vidonge vya kudhibiti uzazi vinaweza kuwa bora kwa wanawake.[9] Isotretinoin ya kumeza kwa kawaida hutumika kwa chunusi kali kwa sababu ya uwezekano wa athari kali.[9]
Matibabu ya mapema na hima hupendekezwa na baadhi ya watu ili kupunguza athari jumla za muda mrefu.[4] Pia limau na asali ni dawa nzuri kwa kutoa chunusi na madoa meusi [11].
Chunusi mara nyingi hutokea katika ubalehe huku ikiathiri takriban asilimia 80–90 ya vijana katika nchi za Magharibi.[12][13][14] Viwango vya chini huripotiwa katika baadhi ya jamii za mashambani.[14][15]
Katika mwaka wa 2010, chunusi ilikadiriwa kuathiri watu milioni 650 duniani kote, hivyo kuufanya kuwa ugonjwa wa 8 unaotokea mara nyingi zaidi ulimwenguni.[16]
Watu pia wanaweza kuathiriwa kabla na baada ya kubalehe.[17] Ingawa hali hii haitokei mara nyingi kwa watu wazima ikilinganishwa na vijana, takriban nusu ya watu katika umri wa miaka ya ishirini na ya thelathini huendelea kuwa na chunusi.[2]
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
|date=
(help)
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chunusi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |