Makerere University
Chuo Kikuu cha Makerere
WitoWe Build for the Future
Kimeanzishwa1922
Ainaumma
ChanselaEzra Suruma
MahaliKampala, Uganda
Kampasimjini Kampala
Tovutihttp://www.mak.ac.ug
Chuo Kikuu cha Makerere

Chuo Kikuu cha Makerere ni chuo kikuu cha kwanza cha Afrika ya Mashariki na chuo kikuu kikubwa cha Uganda.

Kimeanzishwa wakati wa ukoloni mwaka 1922 kama shule ya ufundi kwa wanafunzi 14. Kozi za kwanza zilikuwa pamoja na useremala, ujenzi na umekanika.

Shule ikawa chuo na kozi zikaongezeka kwa masomo ya utabibu, kilimo, maradhi ya wanyama na ualimu.

Kuanzia mwaka 1937 chuo kilianza kozi za stashahada mbalimbali.

Mwaka 1949 Makerere ikawa chuo kishiriki cha Chuo Kikuu cha London kikitoa shahada ya kwanza ya ngazi ya chuo kikuu.

Mwaka 1963 ikawa sehemu ya Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki pamoja na kampasi za Dar es Salaam na Nairobi.

Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki kimegawiwa mwaka 1970 kutokana na kufifia kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Makerere ikawa Chuo Kikuu cha kitaifa cha Uganda.

Chuo cha Viongozi

Makerere ilikuwa chuo waliposoma viongozi wengi wa Afrika, wakiwa pamoja na marais wa zamani Milton Obote (Uganda), Julius Nyerere na Benjamin Mkapa (Tanzania) na Mwai Kibaki (Kenya).

Baada ya uhuru Makerere ilikuwa pia mahali pa majadiliano na mafunzo ya utamaduni wa Kiafrika. Waandishi na walimu muhimu wa Kiafrika walianzisha mafunzo yao au walifundisha kwa muda fulani Makerere kama vile Nuruddin Farrah, Ali Mazrui, David Rubadiri, Okello Oculi, Ngugi wa Thiongo, John Ruganda, Paul Theroux na Peter Nazareth.

Idara

Makerere ina idara 22 zinazohudumia wanafunzi 30,000 hivi, wakiwemo 3,000 wa kozi za shahada za ngazi ya juu.

Vitivo

Taasisi

Vyuo

Idara

Kampasi

Wanafunzi waliopitia Chuo Kikuu cha Makerere

Viungo vya nje