Edith Stein akionekana katika stempu ya Ujerumani.
Edith Stein na mfiadini mwenzake, padri Maximilian Kolbe, wanavyoonekana katika kioo kwa usanii wa Alois Plum huko Kassel.

Edith Stein (12 Oktoba 18919 au 10 Agosti 1942) alikuwa mwanamke mwanafalsafa wa Ujerumani mwenye asili ya Kiyahudi.

Ingawa alilelewa kidini baadaye alipoteza imani hadi alipoanza maisha mapya katika Kristo kwa kubatizwa akawa mtawa wa ndani wa shirika la Wakarmeli. Jina lake la utawani lilikuwa Teresa Benedikta wa Msalaba (kwa Kilatini: Teresia Benedicta a Cruce)[1].

Aliuawa na wafuasi wa Unazi kwa gesi ya sumu katika moja ya makambi ya KZ kule Auschwitz (leo nchini Poland).

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mwaka 1987 halafu mtakatifu mfiadini mwaka 1998 na hatimaye msimamizi mmojawapo wa Ulaya.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 9 Agosti[2]

Maandishi yake

[hariri | hariri chanzo]
Ukumbusho wa Edith Stein huko Prague, Ucheki.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/65800
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Edith Stein
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.