Eneo husika lililokuwa mwaka 830 KK. Edomu inaonyeshwa kwa rangi ya njano.
Ufalme wa Edomu (kwa rangi nyekundu) ulipofikia eneo kubwa zaidi, mwaka 600 KK hivi. Nyekundu iliyokolea inaonyesha mipaka ya kawaida zaidi ya Idumea.

Edomu (kwa Kiebrania אֱדוֹם, Edom, ʼĔḏôm, yaani "nyekundu"[1]) au Idumea (kwa Kigiriki Ἰδουμαία, Idoumaía; kwa Kilatini Idūmaea) walikuwa taifa la Kisemiti lililoshi kusini kwa Bahari ya Chumvi katika eneo ambao leo limegawanyika kati ya Israeli na Yordan.

Biblia inawataja mara nyingi kama washindani wa taifa la Waisraeli[2]ambao walikuwa na undugu kutokana na mababu wao kuwa watoto pacha wa Isaka, mwana wa Abrahamu.

Mataifa hayo mawili yaliendelea kushindana mpaka Edomu ilipomezwa na Israeli wakati wa Wamakabayo (karne ya 2 KK).

Baada ya hapo, Mwedomu Herode Mkuu alipata kuwa mfalme wa Israeli (37 KK - 4 KK) na kuacha ukoo ulioendelea kutawala kwa kwikwi chini ya himaya ya Dola la Roma kwa mwaka 100 hivi.

Tanbihi

  1. Mwa 25:30
  2. Piotr Bienkowski, "New Evidence on Edom in the Neo-Babylonian and Persian Periods", in John Andrew Dearman, Matt Patrick Graham, (eds), "The land that I will show you: essays on the history and archaeology of the Ancient Near East in honour of J. Maxwell Miller" (Sheffield Academic Press, 2001), pp.2198ff

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Edomu