Elizabeth Michael | |
---|---|
Faili:Elizabeth Michael2016.jpg Elizabeth Michael (Lulu) katika 2016 Africa Magic Viewers Choice Awards Lagos,Nigeria | |
Amezaliwa | Diana Elizabeth Michael Kimemeta 16/4/1995 |
Majina mengine | Lulu |
Mhitimu | Chuo Cha Utumishi wa Umma Tanzania |
Kazi yake | Mwigizaji, mtayarishaji wa filamu, |
Miaka ya kazi | 2000-hadi sasa |
Elizabeth Michael (maarufu kama Lulu; amezaliwa 16 Aprili 1995) ni mwigizaji wa filamu kutoka Tanzania. Mwaka wa 2013 alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival kama msanii bora wa kike kupitia filamu "Foolish Age". Mwaka 2017 alitajwa na Tuzo za Vijana Afrika zifanyikazo nchini Ghana miongoni mwa vijana 100 wa Afrika wenye ushawishi mkubwa.
Elizabeth alizaliwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar Es Salaam Tanzania. Ni mtoto wa Lucrecia Kalugira na Michael Kimemeta.
Baadaye alijiunga na katika shule ya Remnant Academy ambapo alimaliza elimu ya msingi. Alipata kusoma Perfect Vision High School, St Mary's High School kwa ajili ya elimu ya sekondari. Baadaye alijiunga katika Chuo Cha Utumishi Wa Umma Tanzania (TPSC) akisomea kozi ya stashahada ya Rasilimali watu na Utawala (Diploma In Human Resources Management).
Alianza kuigiza akiwa na umri wa miaka mitano mnamo mwaka 2000. Baadae alijiunga na kikundi cha Sanaa Kaole Group ambapo alikuwa pamoja na Steven Kanumba, Vincent Kigosi, Mwanaidi Suka na wengine wengi ambapo aliigiza tamthilia nyingi za runinga kama vile Gharika, Taswira, Zizimo na nyingine nyingi ambapo alikuwa akitumia jina la Lulu ambalo limekuwa maarufu mpaka leo.
Baadae alianza kuigiza filamu akiwa bado na Umri mdogo,a mbapo filamu yake ya kwanza ilikuwa Misukosuko akishirikiana na Jimmy Mponda. Mnamo mwaka 2006 aliigiza filamu iitwayo wema iliyoandaliwa na Game 1st Quality na badae filamu nyingine nyingi kama Family Tears,Ripple Of Tears,Passion,Dangerous Girl na nyingine nyingi.Mpaka sasa amepata kuigiza filamu zaidi ya thelathini
Pia amepata kufanya Igizo la redioni lililoitwa Wahapahapa Akitumia jina la Mainda. lililoandaliwa na Media For Development International wakishirikiana na Ubalozi wa Marekani,Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii pamoja na chuo cha Johns Hopkins University Center For Communication Programs cha Marekani Igizo hilo liliongozwa na mmarekani afanyaye shughuli zake Afrika Bwana Jordan Riber.
Pia Katika mradi huohuo wa Wahapahapa alipata kuigiza katika Video mbili za wasanii Lady Jay Dee iitwayo Shamba na Ya Enika iitwayo Changanya .Mradi wa Wahapahapa ulikuwa na lengo la kuelimisha jamii juu Ya malezi bora Ya mtoto katika kipindi cha ukuaji.
Mnamo August 2013 Lulu alizindua filamu Yake Iitwayo Foolish Age ambayo Ni filamu Yake ya kwanza kuitaarisha mwenyewe.Ilizinduliwa katika ukumbi wa Mlimani City uliopo Dar Es Salaam Na kuhudhuriwa Na mamia ya Watu.Foolish Age ilifanya vizuri sokoni Na ilipata kuonyeshwa katika Tamasha Kubwa La Kimataifa La Filamu Zanzibar (Zanzibar International Film Festival) ,na baadae kuteuliwa kuwania Filamu Inayopendwa na Lulu alishinda Muigizaji wa Filamu Wa Kike Anaependwa kupitia filamu hio katika Tuzo za Watu 2014.
Mnamo Mwaka 2015 Alizindua Filamu Yake ya pili Kama mtayarishaji iitwayo Mapenzi Ya Mungu .Filamu Hio ilionyeshwa katika Tamasha La Filamu La Kimataifa La Zanzibar (ZIFF) na mwaka 2016 ilishinda Filamu Bora Afrika Mashariki katika Tuzo Za Africa Magic Viewers Choice Awards zilizofanyika Lagos Nigeria.
Amewahi Kuwa mtangazaji wa kipindi cha runinga kiitwacho watoto wetu Kinachorushwa na Runinga Ya ITV Tanzania Akiwa na umri mdogo mnamo mwaka 2004-2007
Pia mnamo mwaka 2014 na 2015 alikuwa mtangazaji wa mashindano Ya kutafuta vipaji vya uigizaji Tanzania yaitwayo Tanzania Movie Talents
Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2000's | Zizimo | Lulu | Ilionyeshwa Na Independent Television Tanzania (ITV Tanzania) |
Dira | |||
Taswira | |||
Baragumu | |||
Gharika | |||
Sayari | |||
Tufani | |||
Tetemo | |||
Jahazi | |||
Demokrasia | Ilionyeshwa na Shirika la Utangazaji Tanzania/ Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) | ||
2017 | Sarafu | Jackline Sanga "Jack" | Inaonyeshwa na Maisha Magic Bongo (Dstv) |
Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2009 | Wahapahapa | Mainda | Ilirushwa na Radio One Tanzania |
Mwaka | Filamu | Uhusika | Maelezo/Wahusika |
---|---|---|---|
2005 | Misukosuko Part 2 | Catherine | Jimmy Mponda,Seba and Salama Salmin(Sandrah) |
2006 | Wema[1] | Betty | Akishirikiana na Senga |
2007 | Silent Killer | Akishirikiana na Mohamed Nurdin(Chekibudi),Shumileta | |
2008 | Family Tears[2] | Lindah | Akiwa na Steven Kanumba,Wema Sepetu,Jacqueline Wolper and Richard Bezendhout |
Mtoto wa Nyoka | |||
Lost Twins[3] | Anitha Mdogo | Akiwa na Steven Kanumba,Hashimu Kambi ,Suzan Lewis. | |
2009 | Taste of Love [4] | Akiwa na Aunty Ezekiel ,Blandina Chagula,Mahsein Awadh. | |
Ripple of Tears[5] | Lizy | Akiwa na Steven Kanumba | |
Passion | Akiwa Jacqueline Wolper,Irene Uwoya,Yusuph Mlela,Hashim Kambi | ||
Unfortunate Love[6] | Akiwa na Steven Kanumba,Lisa Jensen,Zamda | ||
Too Late | Akiwa na Mahsein Awadh(Dr Cheni),Tumaini Bigirimana(Fifi),Issa Mussa | ||
Reason To Die | Nyina | Akiwa na Mahsein Awadh (Dr Cheni) | |
2010 | Family Disaster[7] | Julieth | Akiwa na Vincent Kigosi,Diana Kimaro |
Crazy Love[8] | Mwanafunzi | Akiwa na Steven Kanumba,Shamsa Ford,Hemed Suleiman | |
My dreams[9] | Akiwa Vincent Kigosi,Irene Uwoya,Shamsa Ford,Mahsein Awadh | ||
2011 | Birthday Party | Akiwa na Salma Jabu(Nisha) | |
Ritazo[10] | Akiwa na Riyama Ally Na Baraka | ||
Tattoo | |||
Confusion[11] | Besta | Akiwa na Diana Kimario,Hemedi Suleiman | |
2012 | House Boy[12] | Lulu | Akiwa na Wema Sepetu,Kajala Masanja,and Mr Blue |
Woman Of Principles[13] | Linah | Akiwa na Vincent Kigosi and Nargis Mohamed | |
Dangerous Girl[14] | Hidaya | ||
Mtoto wa Mbwa[15] | Nice | Akiwa na Simon Mwakapagata (Rado) | |
Yatima Asiyestahili[16] | Njwele | Akiwa Nice Mohamed(Mtunisy) and Jeniffer Kyaka | |
Oxygen[17] | Akiwa na Sydney, Hashim Kambi,Grace Mapunda | ||
2013 | Foolish Age [18] | Loveness | Akiwa na Diana Kimaro and Hashimu Kambi |
2014 | Family Curse[19] | Akiwa na Hashimu Kambi,Yusuph Mlela,Cathy Rupia | |
2015 | Mapenzi Ya Mungu [20] | Shikana | Akiwa na Flora Mtegoa,Linah Sanga |
2016 | Ni Noma [21] | Angela | Akiwa na Kulwa Kikumba and Isarito Mwakalikamo |
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
((cite web))
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Elizabeth Michael kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |