Sanamu ya Mt. Heimo.

Heimo (pia: Heimerad, Heimrad, Haimrad; Meßkirch, Baden, Ujerumani, 970 hivi - Burghasungen, 28 Juni 1019) alikuwa padri ambaye baada ya kufukuzwa monasterini aliishi bila makao maalumu kwa ajili ya Kristo, hadi alipokwenda upwekeni [1]. Mwenendo wake wa ajabuajabu ulimfanya adharauliwe na kudhulumiwa na wengi, lakini yeye hakupotewa na utulivu wake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Juni[2].

Tazama pia

Tanbihi

  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/91710
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.