Muslim ibn al-Hajjaj (jina lake kamili lilikuwa: Abu al-Husayn ‘Asakir ad-Din Muslim ibn al-Hajjaj ibn Muslim ibn Ward ibn Kawshadh al-Qushayri an-Naysabūrī, lakini alijulikana zaidi kama Imam Muslim; 815 - 875)[1] anajulikana kwa mkusanyiko wake wa Hadithi za Mtume Muhammad unaokubaliwa kuwa mkusanyiko muhimu pamoja ule ya Al-Bukhari. Unajulikana kama Sahih Muslim[2].
Muslim alizaliwa Nishapur katika mkoa wa Khorasan, iliyopo katika Iran ya kaskazini-mashariki ya leo. Kufuatana na mapokeo alikuwa Mwajemi au Mwarabu[3].