Wanajiolojia wakichunguza sampuli za mwamba zilizopatikana kwa njia ya kekee.

Jiolojia (kutoka Kigiriki γῆ ge „ardhi“ na λόγος logos, somo, mafundisho“ = "geologia" - kwa matamshi ya Kiingereza "jiolojia") ni fani ya sayansi inayochunguza maumbile ya dunia na tabia zake za kifizikia na kikemia. Inachungulia pia historia ya dunia na nguvu zinazoendelea kubadilisha maumbile ya dunia.

Neno "geologia" liliwahi kutumiwa mara ya kwanza mnamo 1778 na Mfaransa Jean-André Deluc (17271817).

Jiolojia inatazama mawe na ardhi ikitafuta maelezo kwa umbo na tabia zake kuligana na kanuni za kisayansi.

Kuna masomo madogo ndani ya jiolojia kama vile:

Aina za miamba

Jiolojia inachunguza hasa miamba na kutofautisha aina tatu kufuatana na misingi yake:

Ardhi

Asili ya ardhi ni miamba iliyovunjikavunjika na kuchanganyika na mabaki ya mimea na wanyama waliooza.

Picha

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Jiolojia