Kanuni ya Kirumi ni jina la tangu zamani la Sala ya Ekaristi I ya Misale ya Kanisa la Roma inayotumiwa na Wakatoliki karibu wote kuadhimisha Misa.

Kanuni hiyo imebaki karibu sawa tangu karne ya 7. Inaundwa na mshono wa sala fupifupi zinazotangulia na kufuata simulizi la Karamu ya mwisho.[1]

Mabadiliko ya mwisho yalifanywa na Papa Yohane XXIII[2] halafu hasa na Papa Paulo VI[3] Hata hivyo hati Summorum Pontificum ya Papa Benedikto XVI imeruhusu wanaopenda kutumia kanuni kama ilivyorekebishwa na Papa Yohane XXIII.[4]

Tanbihi

  1. Frank Leslie Cross, Elizabeth A. Livingstone, The Oxford Dictionary of the Christian Church (Oxford University Press 2005), p. 281
  2. Acta Apostolicae Sedis LIV (1962), p. 873
  3. Pope Paul VI, Apostolic Constitution Missale Romanum
  4. Pope Benedict XVI, Motu proprio Summorum Pontificum, art. 1

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kanuni ya Kirumi kama historia yake au maelezo zaidi?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.