Nabii Amosi kadiri ya Gustave Doré.

Kitabu cha Amosi ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), na kwa hiyo pia ya Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Nabii mwenyewe

Tofauti na manabii Eliya na Elisha waliomtangulia ambao hawakuacha maandishi, nabii Amosi (786 - 746 hivi K.K.) ana kitabu chenye mafundisho yake aliyoyatoa katika ufalme wa Israeli (Kaskazini) ingawa alikuwa raia wa ufalme wa Yuda (Kusini).

Hakutarajia kutumwa na Mungu, ila ilimbidi akubali kutabiri kwa niaba yake (7:10-17), hasa kuwa Israeli itaangamizwa na kutekwa na Waashuru utumwani kwa makosa yake dhidi ya imani, haki na kwa kufuata anasa (5-6).

Waisraeli walikataa maneno yake hata wakatendwa kama alivyowatabiria kwa ukali wote (2Fal 17:5-23).

Marejeo

Viungo vya nje

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Amosi kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.