Magofu ya Kolosai.

Kolosai (kwa Kigiriki Κολοσσαί, Kolosai), ulikuwa mji wa mkoa wa Frigia (katika Uturuki wa leo) juu ya mto Lukus, kilometa 22 kusini kwa Laodikea, karibu na barabara kutoka Efeso hadi mto Eufrate.

Umaarufu wake unatokana na barua ambayo Mtume Paulo aliwaandikia Wakristo wa huko, waliokuwa wamehubiriwa Injili na mwanafunzi wake Epafra, mwenyeji wa huko[1], lakini waliaanza kupokea mafundisho tofauti yaliyoonekana na Paulo kuwa ya kizushi kwa kuwa yalipunguza umuhimu wa Yesu Kristo.

Barua hiyo imeingizwa katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo kwa jina la Waraka kwa Wakolosai.

Tanbihi

  1. Catholic encyclopedia: Colossæ

Marejeo

Viungo vya nje

37°47′16.18″N 29°15′41.55″E / 37.7878278°N 29.2615417°E / 37.7878278; 29.2615417