![]()
| |
Eneo - Mji - Mkoa wa Jiji |
88 km² 455.61 km² |
Wakazi (2006-01-01) - Mji - Mkoa wa Jiji - Msongamano (mji/jiji) |
501,158 1,115,035 5695/km² / 2447/km² |
Kanda la wakati | Ulaya ya Kati: UTC+1 |
Latitudo Longitudo |
55°43' N 12°34' E |
Kopenhagen (kwa Kidenmark: København = "Bandari ya wafanya biashara") ni mji mkuu wa Denmark pia mji mkubwa wa nchi na kitovu cha utawala, uchumi na utamaduni.
Kopenhagen iko Zealand (Sjælland) ambacho ni kisiwa kikubwa cha Denmark. Iko karibu na mji wa Malmo katika Uswidi ulio ng'ambo ya mlango wa bahari ya Oresund unaounganisha bahari ya Baltiki na Kattegat kuelekea Bahari ya Kaskazini. Sehemu ndogo ya mji iko kwenye kisiwa cha Amager.
Eneo la Kopenhagen lina miji ya Kopenhagen yenyewe (wakazi 501,158), Frederiksberg (wakazi 91,855), Gentoftev (wakazi 68,623) na wakazi wengine 453,399 katika miji midogomidogo ndani ya wilaya ya Kopenhagen.
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kopenhagen kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |