Kungwi
Kungwi madoa (Bubo africanus)
Kungwi madoa (Bubo africanus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Strigiformes (Ndege kama bundi)
Familia: Strigidae (Ndege walio na mnasaba na bundi)
Nusufamilia: Striginae (Ndege walio na mnasaba na bundi)
Jenasi: Bubo Duméril, 1805

Jubula Bates, 1929
Ketupa Lesson, 1830
Lophostrix Lesson, 1836 Pulsatrix Kaup, 1848
Scotopelia Bonaparte, 1850

Spishi: Angalia katiba

Kungwi ni ndege mbuai wa jenasi mbalimbali za nusufamilia Striginae katika familia Strigidae. Spishi fulani zinaitwa kokoko. Ndege hawa ni wakubwa kuliko bundi na spishi za jenasi Bubo ni miongoni mwa spishi kubwa kabisa za Strigidae.

Kungwi wana mgongo kwa rangi ya kahawa au kijivu pamoja na madoa meupe, na mbele yao ni nyeupe pamoja na madoa au michirizi nyeusi au kahawia. Spishi nyingi zina vishungi viwili vya manyoya vinavyofanana na masikio

Ndege hawa hula mamalia wadogo na wakubwa kiasi hasa (mpaka paa mdogo) lakini ndege, watambaazi na wadudu pia. Kokoko-walasamaki hula samaki hasa. Huwinda usiku.

Kwa kawaida jike huyataga mayai 2 lakini 1-5 inawezekana. Tago lao ni ardhini, mitini, kwenye miamba iliyojitokeza nje na hata kwenye vishubaka vya madirisha.

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Spishi za kabla ya historia

Picha