Sanamu ya Mt. Liseri inayotunza masalia yake.

Liseri (alifariki 540 hivi) alikuwa Askofu wa Couserans (Ufaransa) kwa miaka mingi na ilizuia mji huo usivamiwe na Wavisigothi[1].

Alitokea Hispania na kuwa mfuasi wa Fausto wa Riez.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 27 Agosti.[2]

Tazama pia

Tanbihi

  1. Jacques Sirmond (1789). Conciliorum Galliae tam editorum quam ineditorum collectio, temporum ordine digesta, ab anno Christi 177 ad ann. 1563 (kwa Latin, French). Tomus primus. Paris: P. Didot. uk. 797. 
  2. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Liseri