| |||||
Kaulimbiu ya taifa: Tautos jėga vienybėje! "Nguvu ya Taifa ni Umoja!" | |||||
Wimbo wa taifa: Tautiška giesmė | |||||
Mji mkuu | Vilnius | ||||
Mji mkubwa nchini | Vilnius | ||||
Lugha rasmi | Kilituanya | ||||
Serikali | Jamhuri, serikali ya kibunge Gitanas Nausėda Ingrida Šimonytė | ||||
Uhuru Ilitangazwa Ilitangazwa Ilikubaliwa |
16 Februari 1918 11 Machi 1990 6 Septemba 1991 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
65,303 km² (ya 123) 1,35% | ||||
Idadi ya watu - 2016 kadirio - 2011 sensa - Msongamano wa watu |
2,859,709 (ya 141) 3,043,429 45/km² (ya 120) | ||||
Fedha | Euro (EUR )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
EET (UTC+2) EEST (UTC+3) | ||||
Intaneti TLD | .lt1 | ||||
Kodi ya simu | +370
- | ||||
1 Pia .eu pamoja na nchi za Umoja wa Ulaya |
Lituanya (au Lituania) ni nchi huru iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Ulaya. Inajulikana rasmi kama Jamhuri ya Lituania.
Inapakana na Latvia, Belarus, Polandi na Russia.
Ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.
Lituanya iko kwenye mwambao wa Bahari ya Baltiki.
Lituania kuanzia karne ya 13 ilikuwa nchi huru na imara iliyoteka maeneo mengi; kufikia karne ya 15, ikiwa pamoja na Polandi, ilikuwa kubwa kuliko nchi zote za Ulaya.
Mwaka 1795 nchi hizo mbili zilifutwa, na Lituania ikawa sehemu ya Dola la Urusi.
Mwaka 1918, ikawa tena nchi huru, lakini mwaka 1940 Warusi waliiteka tena.
Miaka 1940 - 1990 nchi ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti.
Baada ya umoja huo wa majimbo 15 kusambaratika, Lituania ilijitangaza nchi huru.
Lituania imekuwa nchi mwanachama ya Umoja wa Ulaya tangu tarehe 1 Mei 2004.
Wananchi kwa asilimia 84 wanaongea Kilituania ambacho pamoja na Kilatvia ndizo lugha hai pekee za jamii ya lugha za Kibaltiki kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Ndiyo lugha rasmi.
Mbali na Walituania asili (86.7%), kuna Wapolandi (5.6%), Warusi (4.8%) na wengineo.
Dini ya wananchi ni Ukristo wa Kanisa Katoliki (77.2%), mbali ya Waorthodoksi (4.9%) na Waprotestanti (0.8%). Wasio na dini yoyote ni 6.1%.
Nchi za Umoja wa Ulaya | |
---|---|
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lituanya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |