Magila ni kata ya Wilaya ya Muheza katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,163 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,758 [2]
Msimbo wa posta ni 21407.
Magila ilikuwa kitovu cha kwanza cha misheni ya Kianglikana ya UMCA ilipoamua kufika barani kutoka Zanzibar mwaka 1868[3]. Wamisionari walianzisha hapa Magila Boys Middle School na Hospitali ya Magila[4].
Jengo ambalo lilikuwa shule ya kwanza Tanganyika bado liko. Kwa sasa kuna shule ya sekondari inayomilikiwa na Kanisa Anglikana inayoitwa Hegongo Holy Cross Sekondary na nyingine inayomilikiwa na serikali inayoitwa Magila Sekondari.
![]() |
Kata za Wilaya ya Muheza - Mkoa wa Tanga - Tanzania |
![]() |
---|---|---|
Amani | Bwembwera | Genge | Kicheba | Kigombe | Kilulu | Kisiwani | Kwabada | Kwafungo | Kwakifua | Kwemingoji | Kwemkabala | Kwezitu | Lusanga | Magila | Magoroto | Majengo | Makole | Masuguru | Mbaramo | Mbomole | Mhamba | Misalai | Misozwe | Mkuzi | Mlingano | Mpapayu | Mtindiro | Ngomeni | Nkumba | Pande Darajani | Potwe | Songa | Tanganyika | Tingeni | Tongwe | Zirai |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Magila kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |