Tunapaswa kutunza mazingira yetu kwa sababu kilimo, ufugaji mvua, n.k. huathiriwa na uchafuzi wa mazingira. Mazingira hutunzwa kwa njia mbalimbali kama vile kupanda miti kwa wingi, kutunza vyanzo vyetu vya maji, na kutumia maji vizuri, hasa katika shughuli za kilimo, ili kuliepuka tatizo la ukame.
Kanuni kuhusu ulinzi wa mazingira
Nchi mbalimbali zina kanuni za ulinzi wa mazingira. Kwa mfano katika nchi ya Marekani, kuna kanuni kuhusu ulinzi wa wanyama wanaokaribia kutoweka. Kanuni hii iko katika sheria ya Endangered Species Act (ESA) iliyopitishwa na raisRichard Nixon mwaka 1973. Pia kuna mkataba wa kimataifa uitwao Convention on International Trade in Endangered Species of Wild Flora and Fauna (CITES).
Barani Afrika, ulinzi wa mazingira waendeshwa pia japo kuna majangili wanapenda sana kukiuka sheria ili wajitajirishe kwa kuwinda wanyama kiharamu.
Mazingira ya mezani, graphical user interface kwa kompyuta
Mazingira yanayobadilikabadilika, sera ya kutambulisha mchakato wa kimazingira
Mwingiliano wa maendeleo ya mazingira, aina ya programu za kompyuta ya kusaidia katika kuendeleza wataalamu wa kompyuta ili kutengeneza programu
Mazingira ya wakati, hali ya mashine isiyo halisi ambayo inatoa huduma ya kuprogramu michakato au mipango ya kuprogramu wakati kompyuta ikiendelea kufanya kazi