Mshumaa (kwa Kiingereza candle, kutokana na Kilatini candēla, neno ambalo linategemea kitenzi candēre, kuangaza.[1]) ni kifaa cha kuletea mwanga gizani kinachotengenezwa kwa nta au kemikali fulani.
Unaweza kuwashwa pia kwa sababu ya kuleta harufu au joto, au hata kwa kupima muda[2].
Ili kushika mshumaa, tangu zamani vilitengenezwa vinara vya thamani tofautitofauti na hata vilivyopambwa kwa sanaa.[3]
Mshumaa unawashwa kwa kiberiti, halafu unaendelea wenyewe huku ukiyeyuka taratibu.[4]
Mishumaa ya zamani zaidi kati ya ile iliyopo hadi leo ilitengenezwa huko China miaka 200 KK hivi, na ilifanywa kwa mafuta ya nyangumi.[5]
Kabla ya kuvumbua namna ya kutengeneza umeme, mishumaa na taa za mafuta ndivyo vilivyotumika kuleta mwanga, kama ilivyo bado umeme huo usipopatikana.
Lakini katika nchi zilizoendelea, mishumaa inatumika bado kwa mapambo tu, hasa mahali pa ibada au kuhusiana nayo. [6] Muhimu kuliko yote ni mshumaa wa Pasaka.
|accessdate=
(help)
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |