Onesiforo (jina la Kigiriki lenye maana ya "mleta faida") alikuwa mwanamume Mkristo wa karne ya 1 aliyetajwa na Mtume Paulo kwa shukrani katika Waraka wa pili kwa Timotheo 1:16-18.
Sababu ni kwamba alimsaidia sana alipokuwa Efeso, halafu akamfuata hadi Roma mpaka akafaulu kumuona na kumfariji bila kuonea aibu minyororo yake.[1][2][3]
Kwa hiyo Paulo alimtakia huruma ya Mungu pamoja na familia yake.[4]
Inasemekana Onesiforo alipata kuwa askofu wa Kolofon (Asia Ndogo), halafu wa Korintho. Hatimaye alifia dini mjini Parium (karibu na Efeso)[5].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Septemba[6][7] au kesho yake[8].
![]() |
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Onesiforo kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |