Pioni wa Smirna (alifariki Smirna, leo nchini Uturuki, 250 hivi) alikuwa padri aliyefia dini ya Ukristo wakati wa dhuluma ya kaisari Decius[1][2].
Kwa kuwa alitoa hadharani hotuba ya kutetea imani ya Kikristo, baada ya kuonja uchungu wa gereza, alipoweza kufariji na kutia moyo ndugu wengi wakubali kufia dini, akateswa kikatili na hatimaye akachomwa moto.
Hati za kifodini chake zimetunzwa hadi leo[3][4][5][6][7].
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |