Propaganda (lat. propagare kueneza) ni jitihada ya kuathiri mawazo na maoni katika jamii kwenda mwelekeo unaotakiwa na wenye propaganda. Inafanana na njia zinazotumiwa kwa matangazo ya kiuchumi yanayolenga kuuza bidhaa fulani au kusambaza mafundisho ya kidini lakini eneo la propaganda ni kisiasa. Kwa hiyo mara nyingi sehemu muhimu ya propaganda ni kuchora picha baya ya wapinzani au maadui.

Jambo muhimu katika propaganda ni kuonyesha habari jinsi inavyofaa zaidi kwa kuathiri watu si kuonyesha hali jinsi ilivyo au pande mbalimbali ya hali halisi.

Harakati ya kisiasa kama Ukomunisti au Ufashisti zilitumia propaganda kwa kusudi na wakati mwingine kwa mafanikio. Kutokana na historia hii neno propaganda haina maana mazuri. Siku hizi vyama vya kisiasa na serikali wanapenelea kuita idara husika "mawasiliano na umma" (public relations) au "habari" (information).

Kujisomea

Vitabu

Makala