Kifodini cha Mt. Saturnini katika mchoro mdogo wa karne ya 14.

Saturnini wa Toulouse (Patras, Ugiriki, karne ya 3 - Toulouse, Galia, leo nchini Ufaransa, 257 hivi) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki katika mji huo hadi alipouawa katika dhuluma ya kaisari Decius kwa kutupwa chini kutoka mlimani.

Kadiri ya wanahistoria Wakristo[1]. chini ya kaisari Decius (250 BK), Papa Fabian alituma maaskofu 7 kutoka Roma kwenda Gallia (Ufaransa wa leo) wakahubiri Injili: Grasyano huko Tours, Trofimo huko Arles, Paulo huko Narbonne, Saturnini huko Toulouse, Denis huko Paris, Austremoni huko Clermont na Martial huko Limoges.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 29 Novemba[2].

Tazama pia

Tanbihi

  1. The Vetus Martyrologium Romanum (1961) under Die 18 Decembris: Quintodecimo Kalendas Januarii: "Turonis, in Gallia, Sancti Gatiani Episcopi, qui, a Sancto Fabiano Papa primus ejusdem civitatis Episcopus ordinatus est, et multis clarus miracolis obdormivit in Domino".
  2. Martyrologium Romanum

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Saturnini wa Toulouse
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.