Sharjah (Kiar.: الشارقة ash-shaariqah) ni jina la emirati katika shirikisho la Falme za Kiarabu na pia jina la mji mkuu wa emirati hii.
Ina wakazi 636,000 kwenye eneo la 2,600 km² mwambanoni wa Ghuba ya Uajemi.
Sharjah ni utemi mkubwa wa tatu kati ya Falme za Kiarabu. Inatawaliwa na Sheikh Dr. Sultan al-Qasimi.
Mji wa Sharja ina wakazi 519,000 (2003 sensa). Iko karibu na miji ya Ajman na Dubai na yote mitatu imekuwa sasa rundiko la jiji.