Sifredi (pia: Sigfrid, Siegfried, Sigafridus, Sigeferd, Sigurdr; Uingereza, karne ya 10 - Vaxjo, Uswidi, 1045) alikuwa askofu mmisionari kwa miaka 40 au zaidi[1] huko Uswidi anayehesabiwa kama mtume wake kwa kuwa alimbatiza mfalme Olof III[2] na kushirikiana naye kuinjilisha nchi hiyo na Denmark, mbali ya juhudi zake huko Norwei pia[3].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni 15 Februari[4].
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |