Swahili Rap From Tanzania | ||
---|---|---|
![]() |
||
Compilation album ya Wasanii Mbalimbali | ||
Imetolewa | 15 Novemba, 2004 | |
Imerekodiwa | 2002-2003-2004 | |
Aina | Bongo Flava, Hip hop | |
Urefu | 70 | |
Lebo | Out Here Records | |
Mtayarishaji | Mbalimbali |
Swahili Rap from Tanzania ni jina la albamu ya nyimbo mchanganyiko za muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania. Albamu imetoka tarehe 15 Novemba mwaka wa 2004 chini ya kampuni ya Kijerumani maarufu kama Out Here Records. Albamu imetayarishwa na studio mbalimbali jijini za jijini Dar es Salaam. Albamu ina nyimbo kali kibao za miaka ya 2003 na 2004 yenyewe. Nyimbo hizo kama vile Zali la Mentali, Wauguzi, Alikufa kwa Ngoma, Asali wa Moyo na nyingine kibao.[1][2] Hii ndiyo albamu ya kwanza ya nyimbo mchanganyiko za Bongo Flava kupata kutumiwa na mashirika ya kimataifa.