Kambi ya wakimbizi nchini Iraq.

UNHCR ni kifupisho cha United Nations High Commission for Refugees yaani Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi.

Ni chombo cha Umoja wa Mataifa chenye mamlaka ya kulinda jamii isiyo na makazi (wakimbizi). Mamlaka hiyo haijishughulishi na wakimbizi kutoka Palestina, ambao wanasaidiwa na UNWRA.

Shabaha ya shirika hili ni usaidizi kwa wakimbizi duniani. UNHCR inajenga kambi za kupokea wakimbizi wakati wa vita, inawapatia hifadhi kwenye nchi za jirani, inawasaidia kurudi kwa hiari nyumbani baada ya mapigano au kuhamia nchi nyingine.

Shirika hili lilipokea mara mbili Tuzo ya Nobel ya Amani kwa ajili ya huduma na mafanikio yake ya kuokoa maisha, wakati wa 1954 na 1981.

UNHCR iliundwa mwaka 1950 baada ya vita kuu ya pili ya dunia na makao makuu yake yapo nchini Geneva, Uswisi[1] The UNHCR has won two Nobel Peace Prizes, once in 1954 and again in 1981[2] .

Tanbihi

  1. UNDG Members Archived 11 Mei 2011 at the Wayback Machine.. Undg.org. Retrieved on 2013-07-12.
  2. "Nobel Laureates Facts – Organizations". Nobel Foundation. Iliwekwa mnamo 2009-10-13. 

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
UNHCR