Wanawake wanane wakiwakilisha maradhi ya akili yalivyotambulikana katika karne ya 19 huko Salpêtrière (Paris, Ufaransa). Mchoro wa Armand Gautier.

Ugonjwa wa akili ni tabia ya kuwaza na kutenda namna ambayo ama inasababisha mateso ama walau haifai kukabili maisha halisi.[1] Namna hiyo inaweza kuwa ya kudumu, au kujitokeza mara moja tu au kwa kwikwi au kurudi tena baada ya kuonekana imekwisha.

Aina nyingi za ugonjwa wa akili zimefafanuliwa na kuorodheshwa, kila moja ikiwa na dalili zake za pekee.[2]

Sababu za ugonjwa mara nyingi hazieleweki. Nadharia zinaweza kutegemea utafiti wa aina tofautitofauti. Kwa kawaida ugonjwa wa akili unaelezwa kuchangiwa na jinsi mtu anavyohemka, anavyotenda, anavyowaza na anavyohisi watu, vitu na matukio.[2] Hiyo inaweza kuwa na chanzo katika sehemu fulani ya ubongo, na katika maisha ya kijamii. Fani inayochunguza maradhi hayo inaitwa saikopatolojia.

Huduma kwa wenye ugonjwa wa akili zinatolewa katika hospitali maalumu au katika jumuia chini ya madaktari wa akili, wanasaikolojia na wanasosholojia, wanaotumia mbinu mbalimbali, hasa kutazama na kuuliza maswali. Dawa zinatolewa kadiri ya maagizo ya madaktari hao.[2]

Tanbihi

  1. Stein, Dan J. (Desemba 2013). "What is a mental disorder? A perspective from cognitive-affective science". Canadian Journal of Psychiatry. 58 (12): 656–62. PMID 24331284. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2016-02-03. ((cite journal)): Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Mental disorders Fact sheet N°396". World Health Organisation. Oktoba 2014. Iliwekwa mnamo 13 Mei 2015.((cite web)): CS1 maint: date auto-translated (link)

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Ugonjwa wa akili
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugonjwa wa akili kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.