Ujana ni kipindi cha maisha kati ya utoto na utu uzima.[1][2]
Unaelezwa kama kipindi cha ustawi wa mwili na wa nafsi tangu mwanzo wa ubalehe kwa ukomavu hadi mwanzoni mwa utu uzima.
Ufafanuzi wa umri maalumu wa ujana hutofautiana. Ukomavu wa mtu binafsi huenda unakosa kuwa sawa na umri wao, kwani watu wasiokomaa hupatikana kwa umri wowote.
Umri ambao mtu anahesabiwa ni "kijana", na huduma maalumu chini ya sheria na katika jamii unatofautiana duniani kote.
Vijana karibu wote duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea: kadiri ya UM, kwa sasa ni 85% wa watu wenye umri kati ya miaka 15 na 24, lakini watafikia 89.5% mwaka 2025.
Kila kijana ana wajibu wa kufanya kazi kwa bidii ili maendeleo ya nchi yake yaweze kwenda sawa, kwani kwa kufanya kazi anaepuka zaidi mmomonyoko wa maadili uliokithiri kwa vijana, hasa kuiga mambo ya kigeni yasiyo na manufaa kwao na kwa taifa kwa ujumla.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ujana kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |