Mfano wa chombo cha anga Vostok pamoja na sehemu ya juu ya roketi

Vostok (kwa Kirusi Восто́к, mashariki) ilikuwa jina la mradi wa kwanza wa usafiri wa anga-nje uliofaulu kupeleka binadamu kwenye anga-nje na kuwarudisha tena salama.

Ilikuwa mradi wa Umoja wa Kisovyeti ulioshindana na mradi wa Mercury wa Marekani. Mwanaanga Yuri Gagarin alikuwa binadamu wa kwanza aliyerushwa juu katika chombo Vostok 1 tarehe 12 Aprili 1961 na kuzunguka dunia mara moja katika anga-nje kwa kimo kati ya kilomita 315 na 169.

Mradi wa Vorstok ilikuwa na safari sita za kupeleka wanaanga nje ya angahewa ya Dunia kati ya 1961 na 1963; safari ndefu ilidumu siku tano ambapo Vostok 6 ilimpeleka mwanaanga Valentina Tereshkova aliyekuwa mwanamke wa kwanza katika anga-nje.

Mradi ulitumia roketi za kijeshi zilizobeba chomboanga chenye sehemu mbili

Wakati wa kurudi wanaanga walirushwa kutoka dambra wakarudi ardhini kwa parachuti.