Wakristo wa Kiyahudi walikuwa Wayahudi waliomuamini Yesu kuwa ndiye Masiya (Kristo) aliyetabiriwa katika dini yao.[1]
Mwanzoni Kanisa la wafuasi wa Yesu liliundwa na watu wa namna hiyo karibu peke yao, lakini kadiri miaka ya karne ya 1 ilivyozidi kwenda, waamini kutoka mataifa mengine waliongezeka hadi kuwazidi hao wenye asili ya Kiyahudi.
Hatimaye Wakristo wa Kiyahudi walionekana kundi dogo la watu waliozidi kuzingatia mno mambo ya Agano la Kale, tofauti na Wakristo wenzao[2][3]; kwa mfano: tohara, Sabato na ibada za sinagogini[1][4][5].[6] Tofauti kati yao na Wayahudi wengine ilikuwa tu imani kuhusu Yesu.[7]
Baadhi yao walisisitiza umuhimu wa desturi za Kiyahudi kiasi cha kudai hata Wakristo wenye asili ya mataifa wazifuate[8], lakini Mtaguso wa Yerusalemu (Mdo 15:6-35) uliamua tofauti[8], wakaendelea kumpinga Mtume Paulo na kuvuruga kazi yake ya uinjilishaji wa mataifa.
Wakristo wa Kiyahudi walidhoofisha sana na Vita vya Wayahudi kwa ajili ya kujikomboa (66-135), na maangamizi ya Hekalu la Yerusalemu (70) pamoja na itikadi kali ambayo iliongoza Uyahudi baadaye na kufukuza Wakristo wote kutoka sinagogini.
Hatimaye hata Kanisa la Yerusalemu lilibaki mikononi mwa Wakristo wasio Wayahudi kwa asili.
Pamoja na hayo, mwelekeo wa kutaka Wakristo wafuate masharti mengi au hata yote ya Torati umeendelea hadi leo katika madhehebu mbalimbali.[8]
|accessdate=
(help)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Wakristo wa Kiyahudi kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |