Safari ya Sultani Mansa Musa ya kutembelea Mecca mnamo 1324 akiwa na dhahabu ilivutia sana Mashariki ya Kati na Waislamu wa Afrika Magharibi kwa Wamandinka.

Wamandinka (pia wanajulikana kama Mandenka, Mandinko, Mandingo, Manding au Malinke)[1] ni jina la kabila kubwa huko Afrika ya Magharibi. Wanakadiriwa kufikia milioni kumi na moja (makundi mengine makubwa ya kikabila katika eneo hilo ambao hawahusiani ni pamoja na Wafula, Wahausa na Wasonghai). Wamandinka ni kizazi cha Dola la Mali, ambao walitamba sana wakati wa utawala wa mfalme wa Kimandinka Sundiata Keita.

Marejeo

  1. Godfrey Mwakikagile (2010). The Gambia and Its People: Ethnic Identities and Cultural Integration in Africa. New Africa Press. ku. 43–44. ISBN 978-9987-16-023-5. 

Jisomee

Viungo vya Nje