Vidubini (kwa Kiingereza: microorganism au microbe) ni jina la kundi la viumbehai vidogo sana. Kidubini hakionekani kwa macho bali kwa msaada wa kitambo kama hadubini pekee.
Vidubini ni kundi lenye tabia tofauti sana kati yao. Vingi vyao vina seli moja pekee lakini kuna pia vidubini vyenye seli kadhaa kama vile kuvu na algae. Tabia ya pamoja ni udogo pekee.
Kati ya vidubini kuna
Aina nne za kwanza zinaweza kuishi peke yao au ndani ya miili ya viumbehai wengine. Virusi huongezeka ndani ya viumbehai hao pekee. [1][2][3]
Wataalamu wengine hawahesabu virusi kati ya vidubini kwa sababu si viumbehai kweli.
Vidubini ni muhimu sana katika mchakato wa uhai; algae ya diatomi zinatekeleza sehemu kubwa ya usanisinuru duniani ambayo ni msingi wa lishe ya mimea na wanyama wengi.
Vidubini vingine ni vidusia au pathojeni za magonjwa ya kuambukiza.
Kwa jumla idadi ya vidubini ni kubwa kabisa kuliko viumbehai wote wengine na asilimia 70 za biomasi duniani ni vidubini. Maana yake ni kwamba kwa pamoja viumbe hivi vidogo visivyoonekana kwa macho ni vizito kushinda wanyama na mimea yote ya dunia.
Vidubini vinapatikana kila mahali pa dunia hata kwenye tako la bahari, ndani ya miamba ya ganda la dunia au kwenye ncha za milima marefu hata zikielea katika hewa.
Vidubini ni muhimu katika lishe ya viumbe vingine; vinatekeleza kazi ya kuozesha mata hai iliyokufa (mimea, maiti, mizoga) na kuibadilisha katika hali inayoweza kutumiwa na mimea.
|title=
(help)
|title=
(help)
|title=
(help)
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kidubini kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |