Ajali (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: "accident" au "uninentional injury") ni tukio maalumu linalotambulika na lisilotarajiwa, geni na lisilotakikana ambalo hutokea katika muda na mahali fulani bila sababu au makusudi dhahiri, lakini husababisha madhara yaliyo wazi, hasa vifo.
Ajali hudokeza kwa ujumla matokeo mabaya ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa na kurekebishwa kabla ya tukio hilo.
Wataalamu katika nyanja za kuepuka majeraha hawatumii neno 'ajali' kuelezea matukio ambayo husababisha majeraha katika jaribio la kubainisha asili ya majeraha mengi ambayo yangeweza kukingwa. Matukio kama hayo huzingatiwa kutoka mtazamo wa epidemiolojia - yanaweza kuepukwa na kukingwa. Maneno yanayopendelewa huweza kulifananua tukio lenyewe zaidi, badala ya asili yake isiyotakikana (k.m kugongana, kufa maji, kuanguka, n.k)
Ajali ya aina ya kawaida (magari, moto, n.k.) huchunguzwa ili kubaini jinsi ya kuepukana nazo katika siku zijazo. Mara nyingine hii hujulikana kama uchambuzi wa sababu ya asili, lakini haihusu ajali ambazo haziwezi kutabiriwa. Sababu haswa ya ajali ya nadra isiyoweza kuepukwa huenda ikawa haiwezi tambulika, na hivyo matukio ya siku zijazo yatabaki kuwa "ajali."
Unapofafanua kinaganaga, ajali huweza kutaja tukio lenyewe pekee, bila kuzingatia mazingira ya tukio hilo, au athari za tukio hilo, yaani "ajali" huishia katika tukio la mara moja, ambalo huleta athari ambazo hazikutarajiwa.
Hata hivyo, katika matumizi ya kawaida, 'ajali' huenda ni pamoja na mfumo mzima wa mazingira (fursa, iliyokuwepo awali, au matokeo yanayojiendeleza bila kuthibitishwa; matokeo ya kawaida; wakati na mahali yasiyoweza kutabiriwa; washiriki n.k.) yanayoelekea, pamoja na kusababishwa na tukio hilo.
Mifano ya kimaungo ni kama migongano isiyotarajiwa au maanguko, kujeruhiwa kwa kugusa kitu kikali, moto, au umeme, au kunywa sumu.
Mifano ya ajali isiyo ya kimaungo ni kama kutoboa siri bila kutaka au kusema kitu kimakosa, kusahau miadi, n.k.
Tunatakiwa tuendeshe vyombo vya usafiri kwa uangalifu ili kupunguza ajali, kama vile:
Kwa majeraha ya kimwili yanayopeleka watu kulazwa hospitalini, nyingi huwa ni ajali za barabarani na kuanguka.