Fuko | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Fuko wa Damaraland (Fukomys damarensis)
| ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 6: |
Mafuko hawa ni wanyama wa familia Bathyergidae ambao wanachimba katika ardhi na kushinda takriban maisha yao yote chini ya uso wake. Wanyama wengine waitwao fuko ni wanafamilia wa Chrysochloridae (oda Afrosoricida), Spalacidae (Rodentia), Talpidae (Soricomorpha) na Notoryctidae (Notoryctemorphia). Spishi zote za Bathyergidae zinatokea Afrika kusini kwa Sahara. Hula mizizi, matunguu na viazi. Kwa hivyo wanyama hawa wana meno manne makubwa mbele mdomoni. Huyatumia meno haya pia kwa kuchimba mahandaki yao. Macho na masikio yao ni madogo na mkia vilevile. Wamepoteza nusra uwezo wa kuona, lakini angalau spishi mbili wanaweza kuhisi nuru. Manyoya yao ni kama bahameli na yana rangi ya kahawia au hudhurungi, lakini fuko uchi hana manyoya. Takriban spishi zote huishi peke yao lakini fuko uchi na fuko wa Damaraland ni mamalia wa pekee ambao huishi kwa jamii za aina ya eusocial kama nyuki au mchwa. Jike mmoja na dume mmoja tu huzaa; wanyama wengine wa jamii ni gumba na husaidia kwa kutafuta chakula na kutunza makinda.