Imam Ali akiteka Jinn, Ahsan-ol-Kobar (1568) Golestan Palace

Jini ni jina la Kiswahili lililotokana na neno la Kiarabu الجن‎, al-jinn.

Majini ni viumbe wanaosadikika kuishi katika mazingira ya kila aina; pia baadhi ya watu wanaamini majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kufanya vitu tofautitofauti, pia wenye uwezo wa kujibadilisha kuwa katika hali waipendayo. Asili ya imani hiyo haijajulikana vizuri, lakini ilikuwepo Uarabuni kabla ya Muhammad.

Kwa asilimia kubwa wenye imani ya uwepo wa majini wanasema ni viumbe wasioweza kuonekana, hivyo ni vigumu kupata uthibitisho wa moja kwa moja kuhusiana na viumbe hao. Kadiri ya imani hiyo majini waliumbwa na Mungu kwa kutumia moto na wakiwa wa jinsia mbili; walikuwepo tangu Adamu kuumbwa, hata enzi za Yesu majini walikuwepo, mpaka alipokuja mtume Muhamad.

Uislamu huamini kuna majini wazuri na majini wabaya kwa maana ya madhara yao katika maisha ya mwanadamu na badhi ya Waislamu (pengine wasiofuata misingi sahihi ya Uislamu) hufuga majini hao katika nyumba zao au miili yao na kuwafanya viumbe hao kama wasaidizi au walinzi wa maisha yao kwa wale ambao huamini ni majini wazuri. Lakini wengine hutumia pia majini waitwao wabaya kuharibu na kutesa maisha ya watu wengine kwa kuwatuma kuwaingia miilini na kuleta magonjwa, kuharibu kazi au biashara ya mtu na hata familia.

Hata wasio na dini na baadhi ya Wakristo hutumia majini kuponya wagonjwa na vilema na kufanya miujiza mbalimbali kama kwa mazingaombwe. Pia wapo Wakristo ambao huwatumia majini hao katika mambo yao kama vile kutafuta mali, watoto n.k.

Pamoja na hayo, Ukristo kwa jumla haupatani na imani hiyo, ila kuna madhehebu kadhaa ya Kikristo ambayo huamini uwepo wa majini kwa kuwasawazisha na mashetani. Hivyo kwao hakuna jini mzuri bali wote ni wabaya kwa kuwa wao na mashetani ni sawa, hivyo ni adui wa Mkristo yeyote yule kama alivyo Shetani mwenyewe. Wakristo wa madhehebu hayo wamekuwa wakifanya maombi kwa watu ambao wanadhaniwa kuteswa na majini ili kuwafungua kutoka katika nguvu zao za uovu, sawa na pepo ambao Bwana Yesu (mleta habari njema, yaani Injili) aliwatoa miilini mwa watu na kuwapa wanafunzi wake (wafuasi wake ambao ni Wakristo leo) mamlaka na uwezo wa kuwatoa pia.

Kwa ujumla wake, Mungu Mmoja aliye mfalme wa siku ya malipo, anaweza kukuepusha na kila jambo baya hapa duniani pasipo kuangalia wewe ni wa dini gani. Viumbe vyote ni vya Mungu na ndiye asili ya vyote, nasi tutarejea kwake.

Katika Uislamu

Kadiri ya Uislamu majini ni viumbe wa Allah kama walivyo binadamu, hivyo wanazaa, wanazaliwa na kukua, wana jinsia mbili, wapo wanamtii Mungu na waliomuasi, wana tabia kama za kwetu (uongo, dhuluma n.k.). “Na tulimuumba mtu kwa udongo unaotoa sauti unaotokana na matope yaliyotiwa sura. Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto” (Alhijra 26-27)

Kazi yao wote ni kumuabudu Mungu: “Na sikuwaumba majini na watu ila waniabudu mimi” (Adh-dhaariyaat, 51 au 56).

Tofauti ni kwamba:

Ingawa wapo wanaoamini uwezekano wa majini kutengenezwa na watu, imani inaukanusha. “Sema: Mwenyezi Mungu ndiye muumba wa kila kitu na yeye ni mmoja mwenye kushinda” (Raad 16). Isipokuwa Waislamu wanaamini uwezekano na kuwatumia majini kwa namna mbalimbali.

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Jua habari zaidi kuhusu Jini kwa kutafuta kupitia mradi wa Wikipedia Sister
Uchambuzi wa kamusi kutoka Wikamusi
Vitabu kutoka Wikitabu
Dondoo kutoka Wikidondoa
Matini za vyanzo kutoka Wikichanzo
Picha na media kutoka Commons
Habari kutoka Wikihabari
Vyanzo vya elimu kutoka Wikichuo
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.