“Keep Ya Head Up” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Tupac Shakur kutoka katika albamu ya Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z. | |||||
B-side | I Wonder If Heaven Got a Ghetto | ||||
Imetolewa | 28 Oktoba 1993 | ||||
Muundo | 12" single | ||||
Imerekodiwa | 1992 | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 4:22 | ||||
Studio | Interscope | ||||
Mtunzi | Tupac Shakur | ||||
Mtayarishaji | DJ Daryl | ||||
Certification | Gold (RIAA) | ||||
Mwenendo wa single za Tupac Shakur | |||||
|
"Keep Ya Head Up" ni jina la kutaja kibao kikali cha mwaka wa 1993, ambacho kilitolewa na msanii wa muziki wa hip hop Tupac Shakur. Kina gusia hasa masuala yanayohusiana na ukosefu wa nidhamu kwa jinsia ya kike, hasa kwa wale wakina-mama maskini - weusi. Kibao kina ujumbe maridhawa na mara kwa mara hutumiwa kama mfano wa upande mwepesi au laini wa Shakur.
Wengi huhesabia moja kati ya nyimbo za rap za huzuni ambazo hazijawahi kutengenezwa na mara kwa mara hutujwa na wasanii wengine kwenye kazi zao, inajenga utu wa Shakur kama rapa mwenye kujitambua na mwenye athira kubwa ya muziki wa rap, amepigiwa kura #11 kwenye 100 Bora ya Nyimbo za Rap za About.com, pamoja na "Dear Mama" imepigiwa kura nafasi ya #4.[1]
Ilitolewa kwa mara ya kwanza mnamo 1993 kutoka katika albamu ya Shakur' ya Strictly 4 My N.I.G.G.A.Z., baadaye imeonekana baada ya kifo chake mnamo 1998 kwenye kompilesheni ya albamu yake ya Vibao Vikali. Baadaye ikafuatiwa na wimbo wa Baby Don't Cry (Keep Ya Head Up II) ukiwa kama sehemu ya pili ya kibao hiki - hapo mnamo 1999 na kibao hicho kilitolewa kwenye albamu ya 2Pac ya Still I Rise.
Biti la wimbo huu limechukua sampuli ya wimbo wa Zapp & Roger wa "Be Alright" na kiitikio chake kimechukua sampuli ya wimbo wa The Five Stairsteps' "O-o-h Child", lakini hapo awali ulichukua sampuli ya Big Daddy Kane ya "Prince of Darkness". Kibao kimechukua nafasi ya #2 kwenye chati za Rap nchini Marekani, #7 kwenye chati za Hip Hop/R&B na #12 kwenye chati za Billboard Hot 100.
CDS - maxi single