Kenneth Kaunda

Kenneth David Kaunda (alifahamika pia kama KK; 28 Aprili 1924 - 17 Juni 2021 [1]) alikuwa Rais wa kwanza wa nchi ya Zambia. Alitumikia taifa hilo kuanzia mwaka wa 1964 hadi 1991.

Wasifu

Maisha ya awali

Kaunda alikuwa mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanane. Alizaliwa katika hospitali ya misheni ya Lubwa, kitongoji cha Chinsali, katika Mkoa wa Magharibi mwa Northern Rhodesia, sasa hivi Zambia.

Baba yake alikuwa akiitwa David Kaunda, alikuwa kiongozi wa Kanisa la Kiskoti na mwalimu wa shule za wamisionari, ambaye alizaliwa nchini Malawi na kuhamia Chinsali kwa lengo la kufanya kazi katika Lubwa Mission.

Alianza masomo kadhaa katika Munali Training Centre ya mjini Lusaka (kunako Agosti 19411943).

Kaunda pia aliwahi kuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi na bweni ya Upper Primary School kuanzia mwaka wa 1943 hadi 1945. Alianza kazi ya ualimu huko Lubwa na kuelea zake mjini Lusaka kwa lengo la kuwa mwelekezi wa jeshi, lakini kwa kazi hiyo ilikwisha.

Kuna kipindi alikuwa akifanya kazi katika Migodi ya Salisbury na Bindura. Mnamo mwaka wa 1948, akawa mwalimu katika shule ya mjini Mufulira kwa ajili ya United Missions to the Copperbelt (UMCB). Pia aliwahi kuwa msaidizi katika Kituo cha Ustawi wa Jamii wa Afrika na Bodi ya Walimu wa Shule ya Mine School ya mjini Mufulira.

Kupigania uhuru

Urais

Kuanguka kwake

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Kenneth Kaunda

Marejeo

  1. https://www.aljazeera.com/news/2021/6/17/zambias-founding-president-kenneth-kaunda-dies-aged-97
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kenneth Kaunda kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.