Umoja wa Afrika (UA) (kwa Kiingereza: African Union (AU); Kifaransa: Union Africaine (UA); Kihispania: Unión Africana (UA) ; Kireno: União Africana (UA) ) [1] ni muungano wa nchi 55 za Afrika ulioanzishwa mnamo Julai 2002.
Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002.
Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, rais mmoja, sarafu moja, n.k.
Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, Ukimwi, n.k.
Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa Moroko, iliyokuwa imejiondoa mwaka 1985 kwa sababu UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi huru wakati Moroko inadai ni eneo la majimbo yake ya kusini). [2][3]
Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.
Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni N. Dlamini-Zuma.
Spika wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Roger Nkodo Dang.