Kihispania duniani leo.

Kihispania (español; Kiingereza: Spanish) ni lugha ya kimataifa ambayo ni lugha ya kwanza kwa watu milioni 493; kwa jumla pamoja na wasemaji wa Kihispania kama lugha ya pili kuna milioni 568 duniani wanaosema vizuri Kihispania.

Historia ya lugha

Asili ya lugha hiyo ni katika nchi ya Uhispania (Ulaya kusini magharibi), lakini kutokana na historia ya ukoloni na ya biashara lugha hiyo imesambaa sana, hasa Amerika ya Kusini na ya Kati.

Lugha iliyozaa Kihispania ni Kilatini cha Waroma wa Kale waliotawala kwa muda mrefu Uhispania. Ndiyo sababu maneno yake yanatokana na Kilatini kwa asilimia 80, lakini pia na Kiarabu kwa asilimia 8.

Kati ya lugha za Kirumi Kihispania ni lugha ya kisasa ambayo ni karibu zaidi na lugha ya kale, isipokuwa Kisardinia na Kiitalia.

Nchi zinazotumia Kihispania kama lugha rasmi

Amerika ya Kati na Karibi

Amerika ya Kusini

Afrika

Nchi zenye wasemaji wengi wa Kihispania

Viungo vya nje