Kupatwa kwa Jua (kwa Kiingereza solar eclipse) ni hali ya Jua kutoonekana (au kuonekana kwa sehemu tu) angani wakati wa mchana kwa muda fulani hata pasipo mawingu. Kunatokea wakati mwezi unapita kati ya Jua na dunia na kufunika Jua. Tokeo lake ni kupungua kwa nuru ya Jua hadi kutoonekana kwa muda wa kufika kwa giza wakati wa mchana. Muda wa kufunikwa kabisa ni dakika chache tu.
Kuna utofauti kati ya “Kupatwa kiasi” (ing. partial eclipse) na “Kupatwa kikamilifu” (ing. total eclipse). Kupatwa kwa Jua hutokea kila mwaka, angalau mara mbili hadi mara tano. Lakini kupatwa kabisa kwa Jua hautokei zaidi kuliko mara mbili kwa mwaka.[1][2]. Huonekana katika sehemu za Dunia pekee, si kote.
Kupatwa kwa Jua kunatokea wakati Mwezi unapita kati ya Jua na Dunia. Hapo Jua, Mwezi na Dunia zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu. Katika hali hiyo Mwezi hurusha kivuli chake kwenye uso wa Dunia. Kivuli hiki hakifuniki Dunia yote. Ni kama kinu kwenye uso wa Dunia. Nje ya kivuli hiki Jua linaonekana kwa sehemu au bila upungufu.
Hali ya kupatwa kabisa kwa Jua inatazamwa kila mara kwenye mstari mwembamba kwenye uso wa Dunia, tena giza kabisa kwa muda mfupi. Mstari huu ni njia ya umbra au kitovu cha kivuli chake kwenye uso wa Dunia. Nje ya njia hii kupatwa kwa Jua kunaonekana kisehemu tu katika sehemu zinazoathiriwa na penumbra au kivuli cha kando cha Mwezi. Mbali na njia ya kivuli hiki Jua linaonekana kama kawaida.
Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa Jua.
angalia Mpito wa Zuhura Wakati sayari inapita kati ya Jua na Dunia inafunika sehemu ya Jua. Tofauti haionekani kwa macho lakini inaweza kutazamwa kwa kutumia darubini. Kuna sayari mbili zinazoweza kupita mbele ya Jua kwa macho ya mtazamaji duniani, ni Utaridi (Mercury) na Zuhura (Venus).
|date=
(help)
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kupatwa kwa Jua kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |