Picha yake.

Mena wa Konstantinopoli (mzaliwa wa Aleksandria (Misri), alifariki Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 25 Agosti 552) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 536 hadi kifo chake.

Alipewa daraja hiyo na Papa Agapeto I na hivyo farakano lililotokea wakati wa Papa Vigilio lilikwisha kwa muda fulani [1].

Alitabaruku basilika la Hagia Sofia lililojengwa na kaisari Justiniani I kwa heshima ya Hekima ya Mungu [2].

Anaheshimiwa tangu kale na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 25 Agosti[3].

Tazama pia

Tanbihi

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/67430
  2. http://www.santiebeati.it/dettaglio/67430
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.