Mwangati (Terminalia spp.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mwangati au mpululu
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Miangati ni spishi mbalimbali za mti katika jenasi Terminalia ambazo zina majani madogo kuliko mkungu (Terminalia catappa). Inatokea savana na misitu ya Afrika ya tropiki. Spishi kadhaa, k.m. T. mantaly, hupandwa katika bustani na kandokando ya mitaa. Majina mengine ni mbombaro, mkaa, mkulungo, mpululu, mwalambe, mwarambe na mwavuli. Jina mwangati hutumika pia kwa mti mwingine, Juniperus procera, unaoitwa mtarakwa vilevile.