Nikodemo akisaidia kushusha maiti ya Yesu kutoka msalabani (Pietà, sanamu iliyochongwa na Michelangelo).

Nikodemo (kwa Kigiriki Νικόδημος, Nikodemos) alikuwa mwalimu wa Torati wa madhehebu ya Mafarisayo tena mwanabaraza wa Baraza la Israeli katika karne ya 1 BK.

Anaheshimiwa na Wakristo wengi kama mtakatifu, ingawa sikukuu yake inaadhimishwa katika tarehe tofautitofauti, hasa tarehe 31 Agosti[1].

Nikodemo katika Injili

Anajulikana kwa sababu ya kutajwa mara kadhaa katika Injili ya Yohane,[2] kama mtu aliyevutiwa na Yesu Kristo ingawa aliogopa maneno ya Wayahudi wenzake.

Ndiyo sababu alimtembelea usiku ili kumuuliza maswali ya dini yao bila kujulikana (Yoh 3:1–21).

Baadaye katika baraza alimtetea Yesu kwamba si haki kuhukumu mtu bila kumsikiliza kwanza, lakini alinyamazishwa (Yoh 7:50–51).

Hatimaye alimsaidia Yosefu wa Arimataya kumzika Yesu (Yoh 19:39–42)[3].

Nikodemo katika picha

Tazama pia

Tanbihi

  1. Martyrologium Romanum
  2. Driscoll, James F. "Nicodemus." The Catholic Encyclopedia. Vol. 11. New York: Robert Appleton Company, 1911. 13 Dec. 2014.
  3. , aliyetarajia Ufalme wa Mungu uliotangazwa na Yesu, alichukua jukumu la kumzika

Marejeo

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Category:Nicodemus
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nikodemo kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.