Peloponesi (Kigiriki Πελοπόννησος peloponesos) ni rasi ya kusini mwa Ugiriki. Imeunganika na sehemu ya bara ya nchi kwa shingo la nchi kwenye mji wa Korintho.
Jina la kihistoria la rasi lilikuwa Morea (Μωριάς morias).
Eneo lote la Peloponesi ni kilomita za mraba 21,549. Kuna watu 1,155,000 walioishi huko mwaka 2011.
Peninsula imegawanywa kati ya mikoa mitatu ya kiutawala: sehemu kubwa ni ya mkoa wa Peloponesi, na sehemu ndogo ni za mkoa wa Ugiriki Magharibi na wa Attica.
Ghuba ya Korintho inatenganisha Peloponesi na Ugiriki bara.
Rasi hiyo ina milima mingi na pwani yenye hori ndefu zinazoingia ndani ya nchi. Mlima mrefu ni Taygetos unaofikia mita 2,407 juu ya UB. Rasi yote inakabiliwa na mitetemeko ya ardhi ya mara kwa mara.
Mji mkubwa zaidi ni Patras yenye wakazi 170,000.
Miji mikubwa zaidi ya kisasa kwenye Peloponesi ni (sensa ya 2011):
Rasi hii iliona vipindi na watendaji muhimu katika historia ya Ugiriki ya Kale.
|date=
(help)
Peloponesi travel guide kutoka Wikisafiri
|doi-access=
ignored (help)Makala hii kuhusu maeneo ya Ugiriki bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Peloponesi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |